Thursday, April 30, 2015

Anonymous

NGUO ZA UTUPU NA SNURA WA MAJANGA...MUSTAKABALI HUU HAPA...!

Staa wa Bongo Movies na Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Majanga’, amesema hatavaa nguo za nusu uchi tena kwa kuwa ameshagundua makosa hayo.
Snura alisema awali alikuwa akivaa mavazi ya nusu uchi au nguo za kumbana, lakini kwa sasa amejirekebisha na anatambua nguo zinazompendeza ili kutokuleta sintofahamu kwa mashabiki wake.
“Kiukweli nashukuru ushauri wa watu katika suala la mavazi, nimeshajirekebisha kwa sasa sivai kama zamani mavazi yasiyofaa katika jamii,” alieleza Snura.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.