Kandili Yetu [KY] Ni Blog Inayoongoza Kwa Kukupatia Habari Pendwa Za Mastaa 'UDAKU' wa Bongo Na Ngambo, Matukio, Ya Kitaifa, Kimataifa Siasa, Michezo Na Burudani!
Saturday, March 21, 2015
Anonymous
VIDEO: SUGE KNIGHT AANGUKA MAHAKAMANI BAADA YA KUTAKIWA KUTOA BILIONI 45 KWA AJILI YA DHAMANA
Mwanzilishi wa Label ya Death Row, Mario "Suge" Knight jana alianguka
mahakamani baada ya jaji kumtaka atoe dola milioni 25 ambazo ni zaidi
ya shilingi bilioni 45 za Kitanzania kwaajili ya dhamana kwenye kesi
yake ya mauaji, kiwango ambacho wakili wake amesema ni kikubwa mno. Wakili wa Suge, alisema mteja wake hawezi kumudu kulipa kiasi hicho
cha fedha ambacho Suge aliishiwa nguvu na kuanguka dakika chache baada
ya kusikia taarifa hizo akiwa mahakamani hapo. Awali jaji huyo alidai kuwa ana wasiwasi Suge anaweza kutoroka kwa
kuwa alishawahi kufanya hivyo siku za nyuma. Knight anashikiliwa kwa
kosa la kuwagonga kwa gari watu wawili na kumuua mmoja baada ya kutokea
malumbano.
Note: Only a member of this blog may post a comment.