Mashabiki wa soka wanapofungwa mara
nyingi huchukulia jazba kutokana na matokeo mabaya waliyopata na wakati
mwingine hufikia hatua ya kufanya vurugu ikiwa tu ni kutokana na matokeo
mabaya waliyoyapata.
Hii ilitokea kwa mashabiki wa Real
Madrid ambao walipandwa na jazba na kuamua kulivamia gari aina ya
Bentley lililokuwa linaendeshwa na kiungo Gareth Bale na kulipiga mateke na ngumi kufuatia matokeo mabaya kwa timu hiyo.
Mashabiki hao walikuwa wanamsubiri
mchezaji huyo njiani kwa hamu ya kumvaa wakidai wamefikia hatua hiyo
baada ya Bale kushindwa kuisaidia timu hiyo wakati ikicheza na Barcelona
na kupoteza mchezo huo kwa jumla ya mabao 2-1 kwenye Uwanja Camp Nou.
Inasemekana pamoja na hasira ya kufungwa
lakini pia wamekuwa na chuki ya muda mrefu na kiungo huyo huku
wakiusgutumu uongozi wa klabu hiyo kwa kumnunua kwa gharama kubwa kutoka
Tottenham.
Hata hivyo uongozi wa Real Madrid umewafungia mashabiki wote waliohusika kwenye tukio la kumshambulia mchezaji huyo.


Note: Only a member of this blog may post a comment.