Tuesday, March 24, 2015

Anonymous

Mwanafunzi wa chuo kikuu Dar yamkuta makubwa kisa, mke wa mtu… #Hekaheka MARCH 24

Story iliyosikika kwenye Hekaheka ya leo inahusu ishu iliyotokea maeneo ya Mabibo Hostel ambayo inahusu kijana ambae ni mwanafunzi  wa chuo ambaye kulikuwa na taarifa kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na mke wa mtu. 

Baada ya kukamatwa na mume wa mwanamke huyo, mwanafunzi huyo amesema kuwa mume wa mwanamke huyo alimkuta akiwa ndani kwake akijaribu kumshawishi mwanamke ili alale nae, lakini anajitetea kwamba ni bahati mbaya tu imetokea hivyo. 

Akizungumzia tukio hilo mume wa mke huyo amesema alikuwa amelala akaona message inaingia kwenye simu ya mke wake, alipomuuliza alimwambia hamjui mtu aliyetuma message hiyo.. mwanaume akamwambia amshawishi aje ili amuone. 

Kijana huyo alipofika aliingia ndani na kuanza kumbembeleza mwanamke huyo walale, mwanaume akajitokeza na kuanza kumpiga.. mfukoni alikutwa na condom pamoja na shilingi 600.

Baadaye mwanaume huyo alimpeleka Polisi huku akiendelea kujitetea kwamba ni bahati mbaya imetokea hivyo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.