Friday, March 27, 2015

Anonymous

VIDEO: MAPYA kuhusu mgahawa wa kichina unaotuhumiwa kwa ubaguzi wa rangi Kenya…

Kenya Chinese Restaurant-2
Hii ni story ambayo tangu siku ya kwanza iliposikika toka  Kenya imeendelea kukaa kwenye headlines kila siku, ishu ya kwanza ilikuwa utaratibu ambao mgahawa huo imeuweka, yani ikifika saa 11 jioni hakuna mtu mweusi alikuwa akiruhusiwa kuingia.. Hofu yao ni Al-Shabaab! 

Kingine kilichosikika kuhusu mgahawa huo ni ishu ya lori la mgahawa huo kukutwa katika mtaa wa Kawangware nchini humo likiwa linatupa nyama zilizooza. 

Watu watatu akiwemo mchina mmoja waliokamatwa kwenye gari hilo walifikishwa Mahakama ya kaunti ya Nairobi kujibu mashtaka ya kutupa nyama eneo lisiloruhusiwa. 

Kilichofuatia baada ya hayo ni ishu ya mgahawa huo kufungwa huku wamiliki wakiwa na kesi ya kujibu kuhusu utaratibu ambao wameuweka kuzuia watu weusi kuhusishwa na ubaguzi wa rangi pamoja na kugundulika kufanya biashara bila leseni.  

Manager wa Mgahawa huo Esther Zao jana amefikishwa Mahakamani na kurudishwa gerezani baada ya Mahakama kuzuia dhamana yake. 

Mgahawa huo kwa sasa umefungwa na hakuna mfanyakazi yoyote anayeruhusiwa kuingia, wafanyakazi wa mgahawa huo wamesema walitumiwa ujumbe mfupi uliowataka wasirudi kazini hadi watakapoambiwa wakachukue mshahara wao.

Bonyeza play kusikiliza taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo cha K24 siku ambayo walikamatwa wakitupa nyama zilizooza.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.