Marehemu Kapteni John Damiano Komba.
Stori:GLADNESS MALLYA NA CHANDE ABDALLAH/Risasi HUKU
maelfu ya Watanzania wakiamini kwamba, kifo cha aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM), Kapteni John Damiano Komba ndiyo kile kilichotabiriwa na mnajimu Maalim Hassan Hussein Yahya, mwenyewe ameibuka na kusema sicho!
maelfu ya Watanzania wakiamini kwamba, kifo cha aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM), Kapteni John Damiano Komba ndiyo kile kilichotabiriwa na mnajimu Maalim Hassan Hussein Yahya, mwenyewe ameibuka na kusema sicho!
Akizungumza na Risasi Jumamosi
katikati ya wiki hii jijini Dar, Maalim Hassan alisema kuwa, baada ya
kifo cha Kapteni Komba ambaye alikuwa pia mwanasiasa mkubwa nchini,
wengi wameamini utabiri wake alioutoa mwanzoni mwa mwaka huu kwamba kuna
mtu maarufu mwanasiasa atafariki dunia ghafla, basi ndiye Komba.
“Kwanza nataka watu wajue siyo
Komba. Yule mwanasiasa niliyemtabiria mimi yuko palepale. Yeye ataanguka
jukwaani na atafariki papo hapo,” alisema Maalim.
Aliongeza kuwa, kifo cha Komba
ni upepo wa mauti tu lakini hayumo katika matukio ya utabiri wake wa
mwaka 2015 ambapo alichambua vizuri hali ya kisiasa nchini. Katika
utabiri wake huo, Maalim Hassan alisema mwanasiasa huyo atakuwa mgombea
wa urais (hakumtaja jina lake wala la chama) ambapo atapatwa na mauti
hayo akiwa anahutubia jukwaani kwa ajili ya kampeni.
Kwa madai hayo, wengi walisema
ni Komba kwa sababu katika kipindi cha kifo chake alikuwa anajiandaa na
kampeni za ubunge jimboni mwake na pia alikuwa anajiandaa na nyimbo za
kampeni za kuhamasisha upigaji kura mwaka huu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.