Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amelitaka
Jeshi la Polisi nchini Tanzania kujiandaa kikamilifu ili kukabiliana na
vurugu zozote zitakazojitokeza wakati wa uandikishaji wapigakura,
upigaji Kura ya Maoni ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi
Mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
Akifunga mafunzo ya maofisa
warakibu wasaidizi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Dar es Salaam
jana, Rais Kikwete alisema dalili zinaonyesha kwamba kuna watu wenye nia
ya kuhatarisha amani katika matukio hayo.
Alisema Serikali itahakikisha
kazi ya uandikishaji katika daftari la wapigakura, upigaji wa kura ya
maoni na uchaguzi mkuu vinafanyika kwa amani na utulivu kwa gharama
zozote.
Akikuzungumza katika hafla
hiyo, Rais Kikwete alisema kama serikali inatambua changamoto
zinazolikabili Jeshi la Polisi hasa katika majukumu yake ya kuhakikisha
ulinzi wa raia na mali zake, lakini kazi nzito ikiwa ni wakati huu
ambapo Taifa linaelekea kwenye upigaji wa kura ya maoni kuhusu katiba
inayopendekezwa na uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Raisi hivyo
kulitaka Jeshi la Polisi kutotumia 'maguvu' ili kuifanya amani iendelee
kutawala katika kipindi hiki cha uchaguzi.
Aidha Mwenyekiti wa CUF,
Profesa Ibrahim Lipumba Akizungumzia ya Rais Kikwete, alisema, “Rais
Kikwete yeye ndiye mtu wa kwanza kuivuruga amani kwa kutangaza tarehe ya
kufanyika kwa kura ya maoni wakati siyo jukumu lake na jukumu hilo ni
la Tume ya Taifa ya Uchaguzi "NEC" na serikali yake kushindwa kuratibu
vyema mchakato wa uandikishaji.
Profesa Lipumba amesema, na
hapa tunamnukuu: "Kama uandikishaji hauendi vizuri mpaka sasa, anavunja
sheria za nchi, halafu yeye mwenyewe tena anakwenda kwenye vyombo vya
dola na kuvieleza vijiandae, wakati yeye huyohuyo ndiye ameanzisha
uvunjifu wa amani tunashindwa tumueleweje,” mwisho wa kunukuu.
CHANZO: IRAN SWAHILI PICHA NA MTANDAO

Note: Only a member of this blog may post a comment.