Mchoro wa jengo la hotel hiyo
Mwaka 2013 ujenzi wa hotel ya kwanza Afrika Mashariki itakayokuwa
katikati ya maji kwenye ziwa Victoria ulianza nchini Uganda, huku
ukigharamiwa na serikali ya nchi hiyo.
Hotel hiyo inayotarajiwa kuwa na ghorofa nne, moja ikiwa ni ya
mghahawa, ya pili ikiwa na vyumba vya kulala na mbili zinazosalia ni
kwaajili ya matumizi mengine ilitarajiwa kukamilika baada ya miaka
miwili toka ujenzi uanze.
Taarifa za sasa zinasema kuwa ujenzi huo umesimama kutokana na
ukosefu wa shilingi bilioni 2 za Uganda (zaidi ya 1,252,000,000 TSH)
zinazohitajika kuweza kukamilisha ujenzi huo.
Source: Daily Monitor


Note: Only a member of this blog may post a comment.