Wednesday, March 4, 2015

Anonymous

Kuhusu Profesa J kutangaza rasmi kugombea ubunge jimbo la Mikumi!


Profesa J ametangaza rasmi kuwa atagombea nafasi ya ubunge kwenye jimbo la Mikumi mkoani Morogoro.

Akiongea na 255 ya Clouds, rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Joseph Haule, amesema: Unajua nimeamua kugombea jimbo la Mikumi kwa kuwa hapa ni nyumbani. Wazazi wangu waliishi hapa kwa muda mrefu maana babu yangu alihamia hapa kama miaka 58 iliyopita. Baba pia yupo hapa japo wao ni watu wenye asili ya mkoa wa Ruvuma. Kwahiyo nimeona nimekuwa nikiimba siasa sana naona huu ni muda wa kufanya vitendo zaidi.
-via bongo5

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.