Kutokana na mvua kubwa zilizonyesha DAR na kuleta maafa ya mafuriko kwa baadhi ya sehemu, nyumba ya kifahari ya msanii Diamond Platnumz ambayo ujenzi wake haujakamilika nayo imekumbwa na madhara ya mvua baada ya ukuta wake kuanguka.
Mtaalam wa majengo fundi Saidi amesema
tukio kama hilo linaweza kutokea kutokana ukuta kutowekwa zege la
kutosha chini, na juu inawezekana hapakufungwa mkanda.
Soudy Brown alimtafuta Diamond lakini hakuweza kumpata kwenye simu kwa muda mrefu, akamtafuta meneja wake ambaye ni Said Fella.
Fella
amesema ni kweli ukuta wa nyumba hiyo umeanguka kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha lakini bado iko chini ya mkandarasi na anatakiwa
kukabidhi mwezi wa sita kwa hiyo kuhusu suala la ukarabati liko mikononi
mwao.
Ili kusikiliza story yote bonyeza play hapa chini…


Note: Only a member of this blog may post a comment.