Tuesday, March 24, 2015

Anonymous

Bunge lazungumzia suala la serikali Tatu

Naibu Waziri wa Kariba na Sheria UMMY MWALIMU
Serikali imeliambia Bunge kuwa Muundo wa Serikali tatu uliokuwa unapendekezwa kuwepo kwenye Rasimu ya Katiba ya iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyosimamiwa na Jaji JOSEPH WARIOBA hayakuwa Maoni ya Wananchi walio wengi kama ilivyokuwa inaelezwa.

Naibu Waziri wa Kariba na Sheria UMMY MWALIMU amefafanua hayo Bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ubungo JOHN MNYIKA baada ya MNYIKA kuitaka Serikali kueleza sababu za kuwakataza baadhi ya Viongozi wa Dini na baadhi ya Taasisi kuwaelekeza Wananchi wasiipigie kura ya ndio Katiba inayopendekezwa.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa TAMISEMI AGGREY MWANRI amesema kuwa utekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote nchini huzingatia vipaumbele na Bajeti inayopitishwa na Bunge kila mwaka, sehemu kubwa ya Fedha zinazotumika kutekeleza Miradi hiyo zikitokana na na Ruzuku kutoka Serikali kuu na Mapato ya ndani ya Halmashauri.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.