Tuesday, March 17, 2015

Anonymous

Muigizaji Maarufu Mama G Apagawisha Shindano la Miss Kenya Germany 2015, Lucy Komba Ndani ya Nyumba!

PICHA: Mama G (kushoto) akiwa na Nkalamy na Lucie Komba, zaidi hapo juu. 

Mwigizaji na Mchekeshaji  anaeishi nchini Ugerumani, maarufu kama Mama G for Germany aka Ronet ametoa burudani ya kufa mtu kwenye shindano la  Miss Kenya Germany  2015 lililofanyika usiku wa kuamkia jana huko nchini Ujerumani. 

Mama G aliwavunja mbavu watu kwa vicheko mfululizo wakati alipokuwa akifanya yake ukumbini humo na kulifanya shindano hilo kunoga zaidi. 

Staa wa Bongo Movies ambae kwa sasa anaishi ughaibuni, Lucy Komba pamoja na Rehema Amiry Nkalami wa swahili radio Denmark walikuwa ni moja kati ya watu waliohudhuria kwenye shindano hilo ikiwa ni kumpa support  Mama G. 

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Facebook mama G amewashukuru Lucy na Rehema kwa kuweza kuja kumpa support na kueleza kuwa kuja kwao ilikuwa ni bonge la Surprise kwake.
 na kumtakia mafanikio zaidi kwenye kazi zake za sanaa huko Ughaibuni.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.