Imelda Mtema
STAA wa filamu Bongo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ amekiri kuwa ubize wake katika masomo umemzuia kwa kiasi
kikubwa kupata muda wa kufikiria mambo ya kijinga na hata kujirusha.
Akichonga na paparazi wetu juzikati, Lulu alisema mtu akisimamia
kwenye masomo hawezi kuwa na mawazo mabovu kama ya kwenda kujirusha au
kupata kilevi badala yake unajikuta ukifikiria masomo na mitihani tu.
“Jamani kama mimi sasa hivi sina hata ninachokiwaza zaidi ya masomo
yangu na mitihani ninayokutana nayo yaani hata muda wa kusema utaenda
Club, hakuna nafasi kabisa katika kichwa, hivyo nimeamini kuwa ukiwa
bize na masomo akili za ajabu hazipo kabisa,” alisema Lulu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.