Wednesday, March 25, 2015

Anonymous

Marufuku sigara hadharani TZ !! Sheria mpya ya dawa za kulevya nayo ina mengine hapa.. #PowerBreakfast

radio-dial
Dr. Seif Rashid ametoa tamko la kupinga uvutaji wa sigara katika maeneo ya mkusanyiko wa watu, ripoti mpya ya utafiti imeitaja Tanzania kuwa kinara wa kutengeneza vifaa feki vya umeme Afrika, sheria mpya dawa za kulevya faini bilioni moja au jela miaka thelathini kwa atakayekamatwa nayo, Jeshi la Polisi Kagera linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya watu wenye ulemavu ya ngozi. 

Hali ya siasa ndani ya CCM inazidi kuwa tete baada ya makundi mbalimbali ya jamii kwenda kumshawishi Edward Lowassa agombee Urais. 

Kwenye uchambuzi huo kulikuwa na mazungumzo na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa za kulevya nchini, Godfrey Nzowa ambae amesema sheria mpya ya dawa za kulevya iliyopitishwa na Wabunge ni sahihi kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa.

Hizo zilisikika kwenye PowerBreakfast @CloudsFM, kama ilikupita bonyeza play hapa mtu wangu utasikia zote…

-via millardayo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.