Wednesday, March 25, 2015

Anonymous

HALI TETE CCM

Rais wa Tanzania na mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete.
Hali ya siasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inazidi kuwa tete baada ya makundi mbalimbali ya jamii kwenda kumshawishi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa achukue fomu ya kugombea urais. 

Hali hiyo imedhihirika baada ya makada wa chama hicho kuanza kuvurugana kwa kutoa kauli zinazopingana juu ya wanaomtembelea Waziri Mkuu huyo wa zamani. 

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo, kuwataka wajumbe wa Baraza la Wazazi la chama hicho kuomba radhi kwa kitendo chao cha kwenda nyumbani kwa Lowassa mjini Dodoma na kumtaka agombee urais. 

Pamoja na Bulembo kutoa kauli hiyo, wajumbe hao wamesema hawako tayari kuomba radhi kwa sababu hawaoni sababu ya kufanya hivyo. 

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, wajumbe hao wa Baraza la Wazazi wa CCM, walisema hawataomba radhi kama walivyotakiwa na Bulembo kwa vile walikwenda kwa Lowassa kwa hiyari yao na kwa mapenzi yao binafsi. 

Katika mazungumzo yake, Lupenza alisema viongozi walioratibu ziara hiyo ni pamoja na Katibu wa CCM Wilaya ya Hanang, Vioroka Kajoro na Mjumbe wa baraza hilo Mkoa wa Morogoro, Jackline Ngonyani pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mkoa wa Dodoma, Dk. Damas Mukassa. 

Alisema yeye hakushawishiwa na mtu yeyote kwenda kwa Lowassa ila aliwasikia viongozi hao wakizungumzia juu ya ziara hiyo na kuwataka waweke jina lake kwenye orodha ya watakaokwenda kwa Waziri Mkuu huyo wa zamani.
Niliwasikia wakisema kwa mzee ni saa tatu, nikawauliza mnataka kwenda wapi, wakaniambia wanataka kwenda kumsalimia Lowassa, nikawaambia waniandike na mimi jina. “Kwa hiyo hakuna mtu aliyenishinikiza na hata siku hiyo ya safari, hakuna aliyenikumbusha, kwanza waliniacha nikaenda kwa pikipiki nikiwa nimechelewa,Lupenza 

Ngonyani ambaye amekaririwa na vyombo vya habari akisema alishinikizwa kwenda kwa Lowassa, nilimkuta akiwa nyumbani kwa Lowassa akiwa amekaa kwenye viti vya mbele kabisa.
“Hata wakati wa kupiga picha ulipofika, Ngonyani huyo huyo ambaye sasa ametugeuka, aliwataka wajumbe wengine wote wakae mbali aweze kupiga picha yeye na Lowassa peke yao.
“Yaani hata wakati tunajitambulisha huyo huyo Ngonyani alisema ametumwa na watu wa Ruvuma kumletea salamu Lowassa, kwamba wanamsalimia, sasa anageukaje tena?” 

Kwa upande wake, Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani ambaye ni maarufu kwa jina la Prof. Maji Marefu, alikana kuratibu safari hiyo kama ilivyodaiwa na kueleza kuwa alishirikishwa katika dakika za mwisho na akaamua kwenda.
Wanaojitoa katika ziara hiyo hivi sasa nadhani walifikiri wakienda pale watapewa fedha ama magari. Mimi nimekaa kwenye hii jumuiya kwa miaka 15 sasa, siko tayari kuchaguliwa kiongozi, marafiki wala maadui. Siko tayari kuomba radhi kwa sababu sina kosa nililotenda, nasema sitaomba radhi,Ngonyani. 

Naye Dk. Mukassa alisema yeye aliratibu ziara hiyo kama mwenyeji wa Mkoa wa Dodoma ambaye anapafahamu nyumbani kwa Lowassa. 

Alisema Sh 600,000 walizozitoa kwa ajili ya Lowassa kuchukulia fomu ya kugombea urais, zimetokana na michango yao wenyewe kama wanachama wa kikundi cha kusaidia wajumbe wa jumuiya hiyo.
-MTANZANIA

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.