Monday, March 16, 2015

Anonymous

MARTIN AGEUKA MLEZI MIMBA YA AUNT EZEKIEL!

Imelda Mtema
MWANAMITINDO na meneja wa mwigizaji Wema Sepetu, Martin Kadinda, amenaswa akiwa bize kumhudumia, mwigizaji Aunt Ezekiel ambaye ni mjamzito.

Tukio hilo lilipigwa chabo live na mwanahabari wetu juzikati ambapo Martin alionekana akimchukulia baadhi ya mahitaji muhimu ambayo Aunt alikuwa akiyahitaji kwa wakati huo walipokuwa nyumbani kwa Wema Sepetu, Kijitonyama jijini Dar.

Kama hiyo haitoshi, Kadinda alionekana akilishikashika tumbo la Aunt huku akimtania mara kwa mara.
“Huyu akizaliwa wa kiume itabidi umuite Martin kutokana na ninavyokudekeza hapa,” alisikika Kadinda.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.