Saturday, March 14, 2015

Anonymous

LOVE YA UKWELI: Simba Ukawa wakubali kuishangiliaYanga SC Kesho!

Simba ukawa.
Na Mohammed Mdose,
Dar es Salaam
KUFUATIA kauli ya Yanga ya kuwataka mashabiki wa klabu tofauti za hapa nchini kujitokeza na kuwapa sapoti kwenye mchezo wao wa kesho Jumapili wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Platinum FC ya Zimbabwe, mashabiki wa Simba wa Tawi la Mpira na Maendeleo, maarufu kwa jina la Simba Ukawa, wamekubali kufanya hivyo ila wakatoa masharti.
 

Yanga, kesho inatarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, kucheza na Platinum, mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya michuano hiyo. Ikumbukwe kuwa Yanga imetinga hatua hiyo baada ya kuiondoa BDF IX ya Botswana, huku wapinzani wao wakiitoa Sofapaka ya Kenya. 

Akizungumza na Championi Jumamosi, mwenyekiti wa tawi hilo, Mohammed Kingolile, alisema kuwa wao linapokuja suala la klabu kuiwakilisha nchi, huwa hawana kinyongo na Yanga, hivyo wapo tayari kuishangilia kwa nguvu zote. “Tupo tayari kuwashangilia lakini kauli za kuikejeli Simba alizozitoa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu yao, Jerry Muro, kabla ya mchezo wetu dhidi yao wiki iliyopita, zimetufanya kusita kuishangilia mpaka pale watakapotuomba radhi.”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.