Msanii wa filamu Bongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ ameachana na mpenzi wake wa muda mrefu aitwaye Bonny baada ya jamaa huyo kuweka ‘bondi’ TV yao sambamba na kupewa kipigo pale alipohoji.
Chanzo cha habari kilieleza kuwa, awali Vai na jamaa yake huyo walikuwa wakipendana sana lakini hivi karibuni walizinguana baada ya Bonny kuchukua TV iliyonunuliwa na Vai kisha kuiweka bondi bila kumtaarifu.
“Juzi Bonny kampiga sana Vai, chanzo Vai alihoji sababu ya TV yake kuwekwa ‘bondi’, basi unaambiwa alichezea kichapo na sasa kaamua kumuacha na kurudi kwao,” alisema mtoa habari huyo.Baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Vai ambaye alikiri kuachana na Bonny na kusema: “Ni kweli nimeondoka niko kwetu, vipigo mimi siwezi halafu mtu anakupiga kwa kuuliza kitu ulichonunua mwenyewe.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.