Vijana watatu wakazi wa Manzese Midizini, Dar ambao ni vibaka waliokubuhu, hivi karibuni walimwangukia bibi aliyewapiga mkwara kwamba kwa kuwa walimuibia wasingemaliza mwezi wangekuwa kaburini.
Kwa mujibu wa mtoa kitimbi hiki, vijana hao walimuibia bibi huyo ndoo yake ya kuogea, shilingi 15,000 pamoja na kiredio chake.
“Baada ya bibi kuibiwa vitu vyake alijikongoja hadi kwenye maskani moja ya vibaka akapiga mkwara huo, jioni wale vijana walikwenda nyumbani kwake wakamuomba msamaha na kumrudishia vyote walivyomuibia,” alisema mpashaji wetu.
Aliongeza kuwa, kufuatia sakata hilo baadhi ya wakazi wa eneo analoishi yule bibi walimsifia kwamba alikuwa kiboko ya vibaka pale mtaani.

Note: Only a member of this blog may post a comment.