Tuesday, March 17, 2015

Anonymous

HARUFU MBAYA YA CHOO NDANI YA NDEGE YAZUA MAKUBWA!

ba
Tunafahamu kuwa ndege hulazimika kutua gafla ikiwa katika safari yake pale tu ambapo kunatokea hitilafu ikiwa angani na kusababisha kutua hata kama haijamaliza safari yake. 

Unaweza ukadhani si jambo rahisi lakini hii ni ya kweli imetokea baada ya ndege moja ya shirika la ndege la British Airways kulazimika kutua kufuatia harufu mbaya iliyokuwa ikitokea ndani ya choo. 

Ndege hiyo ilikuwa ikielekea Heathrow Uingereza kutoka Dubai safari ambayo kwa kawaida huchukua saa saba.
pilot
Abiria mmoja aliyekuwa ndani ya ndege hiyo Abhishek Sachdev, aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter kuwa ”ndege yetu ya British Airways imelazimika kurejea dubai baada ya wahudumu kugundua kuwa harufu mbaya inatokea kwenye choo cha ndege hiyo.” 

Rubani wa ndege hiyo alimwita msimamizi wa wahudumu wa ndege hiyo ndipo wakagundua kulikuwa na harufu mbaya ya choo katika safari yao iliyotokea ndani ambayo inaweza kuhatarisha afya zao. 

Alisema ilikuwa ni tayari nusu saa tangu waanze safari na kulazimika kurejea Dubai na hakukua na ndege mbadala ya kuwarejesha London hivyo kusubiri kwa zaidi ya saa 15 .

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.