Monday, March 16, 2015

Anonymous

BREAKING NEWS: MABIBO HOSTEL INAUNGUA MOTO MUDA HUU!

Moto umeibuka katika hostel za chuo cha UDSM zilizoko Mabibo (Mabibo hostel) na bado unaendelea hadi sasa ila chanzo hakijajulikana.

Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho cha UDSM Bwana Gibson George amesema kuwa chanzo hakijajulikana na nini ila moto umesambaa maeneo mbalimbali ya hosteli hizo.

"Watu wa zimamoto tumewapigia mapema sana ila wamechelewa kufika hadi muda huu ndio wamefika, tumejaribu kuuzima moto na umepungua kidogo japo bado unaendelea kwa baadhi ya vyumba" alisema Waziri Mkuu huyo. 
Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea mtandao huu wa kandiliyetu.com

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.