Siwema ambaye ni mzazi mwenzake na Nay wa Mitego alikuwa wa kwanza kuweka post kwenye ukurasa wake Instagram.. aliandika kwamba Curtis ambaye ni mtoto wa Nay sio mtoto wa msanii huyo ila baba yake anaitwa Obasanjo.
Kingine Siwema amelalamika kuhusu Nay ambaye ni mzazi mwenzake kumnyanyasa na pia kuongea vitu ambavyo sio kweli ikiwemo Nay kusema kwamba alimnunulia gari.
Nay muda mfupi aliandika pia kwenye ukurasa wake wa Instagram; “Huyu
ni malaika wa Mungu… Hajui chochote.. Km kuna mtu anasema ni wake aje
amchukue nitampa bila malumbano,, Am a gentleman. Nawapenda wanawake
wote mnaojitambua“– @naytrueboy
Story ya Nay wa Mitego kumchukua
mtoto wake ilisikika kwenye AMPLIFAYA March 17 2015 akisema anamchukua
mtoto wake ili akalelewe na mama yake lakini hana ugomvi wowote na mzazi
mwenzake.

Note: Only a member of this blog may post a comment.