Friday, February 6, 2015

Anonymous

Wabunge "WAPANGA FOLENI" Kuzungumza na Mh. Lowassa Bungeni

Sina uhakika kama Mbunge wa Monduli,Edward Lowassa anaweza kupata nafasi ya kupumzika awapo bungeni.

Ni nadra na mara nyingi haiwezi kutokea kumuona Lowassa akiwa peke yake akipumzika bila ya kuwa na wabunge wengine katika kiti cha pembeni kushoto kwake.

Mara anapoingia ndani ya ukumbi wa bunge,wabunge wengi humfuata kwa zamu na hata kusubiriana wakitaka kuzungumza naye.

Haijulikani ni kitu gani wanachozungumza naye,lakini ukweli ni kuwa Lowassa ni mbunge pekee anayeongoza kuzungumza na wabunge ndani ya ukumbi wa bunge.

Ni jambo ambalo wabunge wengine linaweza kushangaza kuwaona wenzao wakipanga foleni kwenda kuzungumza na kiongozi huyo wa zamani.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU TENA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.