Beki na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Richard Bukos na Abdallah Juma, Tanga
BAO la kichwa lililofungwa kiufundi na beki na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga juzi, lilizua matuko mawili makubwa ambayo ni gumzo mkoani hapa.
BAO la kichwa lililofungwa kiufundi na beki na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga juzi, lilizua matuko mawili makubwa ambayo ni gumzo mkoani hapa.
Kwanza ni Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, kusimama mara baada
ya kuingia kwa bao hilo na pili ni Cannavaro kumkumbatia askari wa kike
wakati akishangilia.
Mara baada ya kupatikana kwa bao hilo katika dakika ya 11, umati wa mashabiki wa Yanga uwanjani hapo ulisimama na kushangilia kwa nguvu, ndipo Kopunovic naye ambaye alikuwa jukwaa kuu, akasimama na kuanza kukuna kichwa chake huku akionekana kutafakari.
Baada ya sekunde kadhaa wakati mashabiki wa Yanga wakishangilia bao hilo, kocha huyo aliamua kukaa kisha akatoa kitabu kidogo alichokuwa nacho na kuendelea kuandika vitu anavyovijua yeye mwenyewe.
Wakati furaha ikiwa haijapoa, Cannavaro alimvaa askari wa kike na kumkumbatia huku ikionekana kama amembusu haraka kisha kuendelea kushangilia na wenzake.
Kitendo hicho kilionekana kuwakera askari wengine waliokuwa karibu na mwenzao huyo na kuonekana kuwa wakali wakizuia mtumishi huyo wa Jeshi la Polisi Tanzania kupigwa picha, lakini askari huyo ambaye alionyesha kutotegemea kilichotokea, alibaki anang’aa macho akishindwa kutabasamu wala kununa.
Alipoulizwa baadaye juu ya kitendo hicho, Cannavaro alisema: “Mimi sikumbusu, nilienda tu kushangilia kwa kumkumbatia kutokana na furaha niliyokuwa nayo, nasisitiza kuwa sikumbusu, hiyo ni hali inayoweza kumkuta mtu yeyote mwenye furaha.”
Awali, Kopunovic alifika uwanjani hapo mapema na kukaa jukwaani, baadaye aliendelea kuufuatilia mchezo huo huku akiandika vitu fulani kwenye kijitabu chake kidogo.
NOMA SANA: BINTI WA MHESHIMIWA MBUNGE ASHUSHA KIWANGO CHA KIPA MANYIKA!
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU
TENA!
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
-Championi


Note: Only a member of this blog may post a comment.