Friday, February 6, 2015

Anonymous

NOMA SANA: BINTI WA MHESHIMIWA MBUNGE ASHUSHA KIWANGO CHA KIPA MANYIKA!

Kipa wa Simba, Peter Manyika Jr. 
KIPA wa Simba, Peter Manyika Jr ameingia kwenye shutuma nzito zinazosababisha kushuka kwa kiwango chake ambapo inadaiwa kuwa uhusiano wa kimapenzi na mrembo mmoja anayejulikana kwa jina la Nima ndiyo sababu. 

Manyika Jr amekuwa akionekana sehemu mbalimbali akiwa na mrembo huyo ambaye inadaiwa ni mtoto wa mbunge, pia picha zao hutawala kwenye ukurasa wa Instagram, lakini baada ya kugundua zimeshasambaa kwa watu mbalimbali, mrembo huyo alizifuta picha hizo. 

Inaelezwa kuwa hali hiyo ya kushuka kiwango imewakera viongozi wengi wa Simba pamoja na baba wa mchezaji huyo Manyika Peter ambaye alimuweka chini mwanaye na kumkanya.

Alipotafutwa na gazeti hili na kusomewa ripoti juu ya taarifa hizo, kipa huyo mwenye umri wa miaka 19, alisema: “Huyo dada ni rafiki yangu wa kawaida na wala sina uhusiano naye wa kimapenzi.  Tatizo letu Watanzania tukiona jambo basi tunalikuza kupita kiasi.” 

Kuhusu picha wakiwa pamoja alisema: “Kweli tulipiga picha lakini hiyo siyo sababu ya kusema kuwa ni mpenzi wangu.”
Alipoulizwa kuhusu kukanywa na baba yake juu ya jambo hilo, alisema: “Kweli baba aliniuliza, nilimueleza ukweli kuwa hakuna kitu kama hicho.” 

Championi Ijumaa lilimtafuta baba mzazi wa kipa huyo, Manyika Peter ambaye alikuwa na haya ya kusema: “Sitaki mwanangu apotee, nilipata taarifa hizo na nikamuita na kuzungumza naye kwa kina lakini aliniambia kuwa yule ni rafiki yake, hata hivyo nikiwa kama mzazi nilimkanya na kumpa mwongozo wa nini anatakiwa kukifanya kufika mbali kisoka.” 

Gazeti hili lilipowasiliana na Nima ambaye inaelezwa ndiye aliyekuwa mrembo katika wimbo wa Mbagala wa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’, naye alifunguka: “Manyika siyo mpenzi wangu ila ni rafiki yangu, najua ana mtu wake kabisa, hiyo video niliyokuwa nimeiweka Instagram tulipiga tukiwa tunatokea mazoezi ya Simba na hata siku hiyo mchumba wa Manyika alikuwa anajua kuwa nipo naye.”
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU TENA!  
-Championi

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.