Chid Benz akitoka mahakamani.
Kesi
inayomkabili mwanamuziki Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ akidaiwa kukutwa na
madawa za kulevya leo imeahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, jijini Dar es Salaam hadi Aprili Aprili 26 mwaka huu.
Kesi
hiyo imeahirishwa baada ya polisi kutowasilisha jalada katika mahakama
ambapo wakili wa serikali, Diana Luhongo, alisema jalada la maelezo ya
awali la mshtakiwa halijawasilishwa mahakamani.
Mwanamuziki
huyo ansdaiwa kukamatwa mwaka jana uwanja wa ndege wa Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya wakati akijitayarisha
kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
ASANTE NA KARIBU
TENA!
(Habari/Picha; Laurent Samatta na Gabriel Ng’osha/GPL)

Note: Only a member of this blog may post a comment.