Stephano Mango, Songea
KIKONGWE Hilda Johnfan Pili (79) aliyepigwa mawe kutokana na imani za kishirikina katika Kijiji cha Kilagano, Peramiho mkoani Ruvuma hivi karibuni, bado hali yake ni mbaya kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata.
KIKONGWE Hilda Johnfan Pili (79) aliyepigwa mawe kutokana na imani za kishirikina katika Kijiji cha Kilagano, Peramiho mkoani Ruvuma hivi karibuni, bado hali yake ni mbaya kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata.
Kikongwe huyo na Maurus Zenda (46) anayedaiwa kuwa ni mwanaye kiukoo,
kwa pamoja walijeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na baadhi ya ndugu zake
kwa kuhisiwa kuhusika katika upotevu wa mtoto Adamu Mselewa (4).
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia wa ukoo huo, hali ya bibi huyo bado ni mbaya na wanajitahidi kwa hali na mali kuokoa maisha yake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma alikolazwa.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Mihayo Msekhela, waliwakamata watuhumiwa 10 kutokana na tukio hilo, ambao ni Ambros Mselewa (24) ambaye ni baba mzazi wa mtoto aliyepotea, Maria Zenda (45), Lameck Zenda (22), Pautas Komba (24), Fredy Mende (24), Gerord Ngonyani (27), Odilo Mwingira (21), Shadrack Ngonyani (22), Hilda Zenda(36) ambao wote ni wakazi wa Kijiji cha Muunganozomba.
Msikhela alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa moja asubuhi baada ya baba mzazi wa mtoto huyo, Ambros Mselewa akiwa pamoja na watu wengine walipoanza kuwashambulia watu hao wakimtaka kijana wao aliyepotea kimauzauza tangu Februari 3, mwaka huu.
PICHAZ: TOP 10 YA WAIGIZAJI WA KIKE WENYE MVUTO AFRIKA!
===>>JIONEE HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
===>>JIONEE HAPA!
ASANTE NA KARIBU
TENA!


Note: Only a member of this blog may post a comment.