Friday, February 20, 2015

Anonymous

MAKUBWA NA MAZITO HAYA: KWANINI MNANIZALISHA?! SNURA MAJANGA ANG'AKA!

Msanii anayefanya muziki na filamu Bongo, Snura Mushi.
Gladness Mallya/Ijumaa
Msanii anayefanya muziki na filamu Bongo, Snura Mushi ameeleza kushangazwa kwake na taarifa zinazozidi kuenea kuwa amejifungua, jambo ambalo anadai eti siyo kweli.

Madai ya staa huyo kujifungua kwa siri yameenea na hata wasanii wenzake wanajua hivyo lakini mwenyewe amekuwa akikanusha na kuwaacha mashabiki wake njia panda.Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni, Snura alisema yeye ana mtoto mmoja mkubwa lakini madai ya kwamba amejifungua hivi karibu hayana ukweli. 

“Mimi sina mtoto mdogo, mwanangu ni yule mnayemjua, hao wanaosema nimezaa mbona wananizalisha?” alihoji Snura ambaye baada ya muda mrefu kupotea, juzikati aliibukia kwenye Ukumbi wa Escape One ulipo Msasani, jijini Dar.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142. 
ASANTE NA KARIBU TENA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.