Tuesday, February 3, 2015

Anonymous

SAD NEWS: AISHA WA MAMBO HAYO ANUSURIKA KIFO AJALINI!

Na Shani Ramadhani/Uwazi 
MKONGWE wa maigizo aliyekuwa akiwakilisha kundi la Nyota Ensemble lililokuwa likitamba na Tamthiliya ya Mambo Hayo, Teckla Mgaya ‘Aisha’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari akiwa njiani kuelekea Moshi. 

Chanzo kinaeleza kuwa gari aina ya Toyota, Land Cruiser liliacha njia na kuvaa gari la akina Aisha na kuwagonga kwa ubavuni upande wa kulia. 

Baada ya kupata taarifa hizi, paparazi wetu alimvutia waya Aisha kujua zaidi ambapo alifunguka;
“Ni kweli tulipata ajali ambayo ilitokea barabara ya Arusha Moshi wakatinikimsindikiza shemeji yangu stendi kuu ya Moshi aliyekuwa akielekea jijini, Mwanza. Hatujaumia na gari yetu ilikuwa katika matengenezo madogomadogo ambayo yameshakamilika.”
PATA HABARI HARAKA ZITUFIKIAPO.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA
 KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142. 
ASANTE NA KARIBU TENA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.