Mchezaji huyo wa Real Madrid hivi karibuni huenda akajikuta akitumiwa katika elimu ya chuo kikuuu baada ya chuo cha British Columbia Okanagan kuanzisha kozi ambayo itakuwa na masomo yanayomhusu nyota huyu .
Chuo hiki kitaanzisha kozi ya shahada ya juu ya Sosholojia (Sociology) ambayo itakuwa inasomwa na wanafunzi kwa muda wa miaka minne huku wanafunzi hao wakijiktia kwenye umaarufu wa nyota huyu na jinsi ambavyo anaathiri watu mbalimbali duniani na utamaduni kwa jumla .
Chuo cha Biritish Columbia Okanagan kilichoko nchini Canada kinataka kuanzisha kozi ya Cristiano Ronaldo .
Profesa Luis Aguilar ambaye ameanzisha wazo hili amesema kuwa Ronaldo ni mtu mwneye umaarufu wa kipekee na ni muhimu kwa watu kufahamu umaarufu wake unavyowagusa watu tofauti duniani.
Umaarufu wa Ronaldo ni muhimu kusomwa na wanafunzi wa kozi ya Sosiolojia kwa mujibu wa Professa wa chuio kikuu cha British Columbia.
Endapo kozi hii itapitishwa na kuanza kutumika rasmi Ronaldo atakuwa mchezaji wa pili wa Real Madrid na Manchester United kutumiwa kama kozi ya chuo kikuu baada ya mchezaji wa zamani wa Madrid na United David Beckham ambaye ametumika katika masomo kadhaa kwenye chuo cha Strefordshire huko Uingereza .
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.
KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
ASANTE NA KARIBU TENA!
-via millardayo


Note: Only a member of this blog may post a comment.