Saturday, February 14, 2015

Anonymous

MECHI YA YANGA NA BDF YA BOTSWANA ILIVYOKUA!

Mshambuliaji Amis tambwe leo ameiongoza Yanga kuichapa timu ya BDF kutoka Botswana katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa awali kuwania kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam, Yanga imecheza kwa kujiamini na kushambulia muda wote na kufanikiwa kupata mabao hayo pamoja ja kosa kosa za hapa na pale.

Mabao ya Yanga yamefungwa katika dakika ya 1 kwa Tambwe kuunganisha mpira wa kona, na dakika ya 56 kwa kuunganisha 'kros' ya Mrisho Ngassa.
Kwa matokeo hayo, Yanga imejiweka pazuri kusonga mbele kwani katika mchezo marudiano utakaopigwa nchini Botswana wiki mbili zijazo, Yanga itahitaji sare aina yoyote.

Kesho Azam itakuwa na kibarua kizito itakapokutana uso kwa uso na El Merreikh kutoka Sudani katika mchezo wa Kwanza wa mzunguko wa awali kuwania Kombe la Klabu Bingwa barani Afrika.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142. 
ASANTE NA KARIBU TENA!
-EATV

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.