Tuesday, February 10, 2015

Anonymous

Mastaa watatu wa soka wanaoongoza kuwa na followers zaidi ya milioni 10 kwenye Instagram

Kwa upande wa mastaa wa soka duniani, mshambuliaji wa Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi amesogea kwenye top three ya wachezaji wa soka wenye followers wengi duniani, Messi ana jumla ya followers milioni 10 katika mtandao wa Instagram. 

Messi anakuwa mchezaji wa tatu duniani kwa kuwa na followers wengi huku akiongozwa na mshambuliaji mwenzake Neymar aliyefikisha followers milioni 15.2 na nafasi ya pili ikishikwa na mwanasoka bora duniani Cristiano Ronaldo ambaye ana watu milioni 12.2
“leomessi10M muchas gracias a todos (Thank you very much to all)“– @

Messi aliweka ujumbe huo kwenye ukurasa wake Instagram pamoja na picha yake akiwa amevaa jezi yenye namba kumi mgononi na maneno “MESSi 10 MILLONES”.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU TENA!  

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.