Na Makongoro Oging’/Uwazi
SIKU chache zomepita tangu Remy Joseph, 35, (pichani) kudaiwa kumuua kwa kumchinja na kisu mkewe, Josephine Mushi kwenye Hoteli ya Friends Corner iliyopo Manzese jijini Dar, mengine yamebainika, Uwazi limechimba zaidi.
Taarifa kutoka vyanzo vya habari hotelini hapo zinadai kuwa, saa tano asubuhi ya Januari 23, mwaka huu, mwanamume huyo alifika kwenye hoteli hiyo na kufanya sherehe ya kuzaliwa kwake ‘bethidei’ ambapo alikuwa akitimiza miaka 35.
Mmoja wa wahudumu wa hoteli hiyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alisema siku hiyo mtuhumiwa huyo alifika akiwa na mwanamke mweupe (jina halikupatikana) ambaye wahudumu wote walijua ndiye mke wake kutokana na kuwa mstari wa mbele katika shamrashamra hiyo.
“Sisi tulimuona ni kijana mstaarabu na haya ya mauaji yasingetokea,
lakini kumbe alikuwa akisherehekea huku akijua atamuua mkewe siku si
nyingi mbele tena kwenye hoteli hiihii, kwa kweli imetushangaza sana,”
alisema mhudumu huyo.
Uwazi lilimtafuta mkurugenzi wa hoteli hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Massawe ambapo alikiri kupata taarifa ya sherehe hiyo kutoka kwa wahudumu wake lakini hakujua alichodhamiria mtuhumiwa huyo mpaka mauaji yalipofanyika na kubainika kuwa, kumbe ni yeye aliyekuwa ameandaa sherehe.
Katika toleo la gazeti hili Namba 880 Februari 3 hadi 9, mwaka huu ukurasa wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa;
HIVI NDIVYO MUME ALIVYOMCHINJA MKEWE HOTELINI.
Joseph alikutwa na polisi katika chumba kimoja cha hoteli hiyo akiwa na kisu mkononi muda mfupi baada ya kumchinja mkewe wake na yeye kutaka kujiua lakini akashindwa.
Ilidaiwa kuwa, Joseph alipanga hotelini hapo Januari 28, mwaka huu huku akiwa na mkewe huyo lakini siku ya pili wahudumu waliona damu zikitiririka kutoka chumbani kupitia mlangoni. Waliita polisi na walipofika walibaini kufanyika kwa mauaji hayo ya kinyama.
Mtuhumiwa bado yupo Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu chini ya ulinzi mkali wa polisi huku mkewe akizikwa Moshi, Februari Mosi mwaka huu.
SIKU chache zomepita tangu Remy Joseph, 35, (pichani) kudaiwa kumuua kwa kumchinja na kisu mkewe, Josephine Mushi kwenye Hoteli ya Friends Corner iliyopo Manzese jijini Dar, mengine yamebainika, Uwazi limechimba zaidi.
Taarifa kutoka vyanzo vya habari hotelini hapo zinadai kuwa, saa tano asubuhi ya Januari 23, mwaka huu, mwanamume huyo alifika kwenye hoteli hiyo na kufanya sherehe ya kuzaliwa kwake ‘bethidei’ ambapo alikuwa akitimiza miaka 35.
Mmoja wa wahudumu wa hoteli hiyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alisema siku hiyo mtuhumiwa huyo alifika akiwa na mwanamke mweupe (jina halikupatikana) ambaye wahudumu wote walijua ndiye mke wake kutokana na kuwa mstari wa mbele katika shamrashamra hiyo.
Uwazi lilimtafuta mkurugenzi wa hoteli hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Massawe ambapo alikiri kupata taarifa ya sherehe hiyo kutoka kwa wahudumu wake lakini hakujua alichodhamiria mtuhumiwa huyo mpaka mauaji yalipofanyika na kubainika kuwa, kumbe ni yeye aliyekuwa ameandaa sherehe.
Katika toleo la gazeti hili Namba 880 Februari 3 hadi 9, mwaka huu ukurasa wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa;
HIVI NDIVYO MUME ALIVYOMCHINJA MKEWE HOTELINI.
Joseph alikutwa na polisi katika chumba kimoja cha hoteli hiyo akiwa na kisu mkononi muda mfupi baada ya kumchinja mkewe wake na yeye kutaka kujiua lakini akashindwa.
Ilidaiwa kuwa, Joseph alipanga hotelini hapo Januari 28, mwaka huu huku akiwa na mkewe huyo lakini siku ya pili wahudumu waliona damu zikitiririka kutoka chumbani kupitia mlangoni. Waliita polisi na walipofika walibaini kufanyika kwa mauaji hayo ya kinyama.
Mtuhumiwa bado yupo Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu chini ya ulinzi mkali wa polisi huku mkewe akizikwa Moshi, Februari Mosi mwaka huu.
AIBU MANCHETER UNITED! Wachezaji Wake Wacheza Mkanda Wa Ngono!
===>>SHUKA NAYO HAPA!
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU
TENA!
===>>SHUKA NAYO HAPA!

Note: Only a member of this blog may post a comment.