Kichwa! Staa bei mbaya wa sinema za Kibongo aliyejizatiti katika masomo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anadaiwa kuwafunika kimasomo wanafunzi wenzake katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kilichopo Magogoni-Posta jijini Dar.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipozi.
Akizungumza hivi karibuni chuoni hapo, mmoja wa wanafunzi wanaosoma
na mwigizaji huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema Lulu amekuwa
akihudhuria vizuri darasani na kufanya vyema kwenye masomo yake
mbalimbali zaidi ya wanafunzi wengi anaosoma nao.“Lulu yupo vizuri sana kimasomo, anawapita hadi wanafunzi wengine. Mahudhurio yake ni mazuri na anafanya mitihani yake na kufaulu.
“Anavaa nguo zinazostahili na hapa chuoni kila mwanafunzi anampenda kwa sababu yupo ‘peace’ ile mbaya,” alisema mnyetishaji huyo na kusisitiza kuwa msanii huyo haishi kama supastaa.
PATA HABARI HARAKA ZITUFIKIAPO.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.
KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
ASANTE NA KARIBU TENA!
Note: Only a member of this blog may post a comment.