Stori Na:Gladness Mallya/Ijumaa Wikienda
MSANII mkongwe katika
gemu la filamu Bongo, Wastara Juma ameapa kumshtaki mtu atakayekamata
kutokana na baadhi ya mashabiki kuwa na tabia ya kumtukana matusi ya
nguoni mtandaoni huku wakimhusisha na marehemu mumewe, Sajuki.

Msanii mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Wastara Juma.
Akizungumza na gazeti hili, Wastara alisema anajisikia vibaya baadhi
ya mashabiki wanavyomtukana kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo siyo
zuri kwani wanaingilia maisha yake binafsi na kibaya zaidi wanamhusisha
Sajuki. “Ukweli sipendi kabisa na nitamshtaki mtu maana wananitengenezea chuki kwani wakati mwingine wananitukana, wanamtukana sana Bondi huku wakidai kwamba nilikuwa naomba Sajuki afe ndiyo nifanye mabaya sasa sijui nimefanya kitu gani kibaya, kuwa na Bondi nimekuwa naye baada ya mume wangu kufariki maana mimi ni binadamu na kama angekuwepo nisingekuwa na mwanaume mwingine zaidi yake,” alisema Wastara.
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU
TENA!

Note: Only a member of this blog may post a comment.