Tuesday, February 10, 2015

Anonymous

HATIMAYE OMMY DIMPOZ, AUNTY WAFUNGUKA KUHUSU PICHA ZA KIMAHABA ZA WEMA NA OMMY ZILIZOVUJA!

Zile picha za mahaba zilizosambaa kwenye mitandao zikimuonyesha Staa wa Bongo Fleva,Ommy Dimpoz na Wema Sepetu wakiwa kitandani zimezidi kuzua utata baada ya Ommy kusema hakujua alipigwa saa ngapi kwani hakuwa na fahamu bali aulizwe Wema.
Ommy akizungumza katika kipindi cha Uheard na Soudy Brown amesema kuwa hana maelezo zaidi ya kuzungumza zaidi ya kusema kuwa hajui ni muda upi zilipigwa picha hizo.
Wiki hii picha hizo zilisambaa mitandaoni na kuzua maswali kuwa Ommy Dimpoz ameamua kujiweka kwa Wema baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platinum.
Hata hivyo, Aunty Ezekiel ambaye ni rafiki wa Wema amesema kuwa rafiki yake huyo alikwenda nchini Afrika Kusini kufanya video mpya ya ngoma ya Ommy.

Wiki pia picha nyingine zilisambaa Wema akiwa na aliyekuwa mume wa Zari wakiponda raha nchini humo na kuzua sintofahamu. Sikiliza U Heard ya leo February 10 kwa kubonyeza play.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU TENA!  

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.