Wachezaji wa Yanga.
Khadija Mngwai na Mohammed Mdose, Dar es Salaam.TIMU ya Yanga imeondoka leo alfajiri kuelekea nchini Botswana kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano dhidi ya BDF XI unaotarajiwa kupigwa keshokutwa Ijumaa katika Dimba la Roberte nchini humo.
Yanga wameondoka na msafara wa watu 31 wakiwemo wachezaji wanne, benchi la ufundi saba pamoja na viongozi wanne lakini kikubwa zaidi pia wameondoka na maji pamoja na chakula chao ambavyo watavitumia kipindi chote watakachokaa nchini humo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, alisema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuwaweka wachezaji wao kwenye hali nzuri ya kimchezo na kuwawezesha kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo.
“Timu inaondoka kesho(leo) alfajiri na wachezaji 20, benchi la ufundi saba pamoja na viongozi wanne na tunatarajia kucheza mchezo wetu Februari 27 saa 19:30 GMT (sawa na saa 11:30 kwa saa za Afrika Mashariki) kwenye Uwanja wa Robate, ambao upo kilometa 70 kutoka Mji Mkuu wa Gaborone.
“Tunaondoka na chakula chetu na hatutarajii kutumia kitu chochote cha kwao, yaani kuanzia chakula, maji hadi usafiri, basi letu litakuwepo huko kwa kuwa litawaleta mashabiki wetu ambao watatupa sapoti kwenye mchezo huo,” alisema Muro.
HABARI NJEMA: CAF yampeleka Msuva wa Yanga Ulaya!
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
ASANTE NA KARIBU
TENA!
-CHAMPIONI


Note: Only a member of this blog may post a comment.