Tukio hilo lililokusanya kadamnasi ‘nzi’ lilijiri juzikati maeneo ya Sinza-Afrika Sana jijini Dar nyumbani kwa wanandoa hao.Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mke huyo alidamka mapema na kwenda kibaruani ndipo mumewe alipoingiza mchepuko ndani.
MKE ATONYWA
Kama kawaida yao wachambua mchele walimgawia punje chache mke wa jamaa huyo aliyekuwa njiani kuelekea kazini kwake wakidai kuwa arudi nyumbani haraka kwa kuwa mumewe alikuwa ameingiza hawara ndani kwake.
Bila kuchelewa, mke huyo alirudi nyumbani haraka na kumkuta mumewe akiwa na mchepuko wake wakiwa bado hawajaanza kufanya chochote lakini kwa pozi alilowakuta nalo liliashiria kuwa kulikuwa kuna uchepukaji kati yao.
TIMBWILI
Mke huyo aliyekuwa hashikiki, aliangusha timbwili la kufa mtu kwa mumewe hali iliyompa nafasi mgoni kutoweka eneo hilo huku timbwili hilo likihamia kwa wifi yake ambaye naye alituhumiwa kumfichia kaka yake maovu.
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo, wanahabari wetu walitinga kwenye eneo la tukio na kujionea hali halisi ambapo wifi mtu alionekana akizungumza na simu muda wote huku watu wakiwa wamejaa eneo hilo.
WIFI AFUNGUKA
Akizungumza na waandishi wetu, wifi mtu alisema kuwa amejikuta akishambuliwa na mke wa kaka yake bila kujali kuwa yeye ni mgonjwa hivyo hastahili kupigwa wala kulaumiwa kwa makosa ya kaka yake.
“Ndiyo kwanza nimetoka kuumwa, hapa sipo sawa.
Nashangaa wifi anakuja kunishambulia eti kwa nini simwambii anachofanya kaka, sasa hata kama ninajua anachofanya kaka yangu ndiyo niingilie mapenzi yao kweli?” alihoji wifi huyo aliyegoma kutaja jina.
MUME AKIMBIA
Mapaparazi wetu waliokuwa eneo la tukio walimtafuta mume ili ajibu mashtaka yake, lakini taarifa zilisema kuwa naye alitoweka baada ya kuona umati unajaa pasipo mtu yeyote kumuona.
POLISI ATIMBA
Polisi aliyevalia nguo za kiraia alifika na kumuamuru mke na wifi yake kupanda kwenye Bajaj na kuelekea Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa ajili ya mahojiano zaidi. Mke, akiwa kwenye Bajaj hiyo aliwashutumu polisi kwa kuwahi kumkamata yeye badala ya kumkamata mumewe aliyemfumania muda mfupi uliopita.
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU
TENA!


Note: Only a member of this blog may post a comment.