Wednesday, February 4, 2015

Anonymous

BALAA! Jordan walipiza kisasi baada ya rubani wao kuuawa na kundi la Islamic State kwa kuchomwa moto!

Sajida al-Rishawi
Serikali ya Jordan imewauwa wapiganaji wawili wa kiislamu, waliokuwa wamezuiliwa korokoroni nchini humo na ambao Islamic State ilitaka wabadilishane na rubani aliyechomwa moto pamoja na mwanahabari wa Japan ambaye aliuwawa juma lililopita.

Msemaji wa Serikali Mohammad al-Momani, amesema kuwa waliouwawa ni mlipuaji mmoja wa kike raia wa Iraqi Sajida al-Rishawi na mfuasi wa Al-Qaeda, Ziad al-Karboli.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameungana na mataifa mbalimbali duniani kulaani mauaji ya rubani huyo yaliyofanywa na kikundi cha Islamic State, ambacho pia kinajulikana kama Daesh.

Rubani huyo alikamatwa ndege yake ilipoanguka katika makabiliano na wapiganaji wa IS nchini Syria mwezi Disemba.
Jordan ilijaribu kumuokoa luteni Kasasbeh katika ubadilishanaji uliomuhusisha Rishawi.


Alikuwa amehukumiwa kunyongwa kufuatia msururu wa mashambulizi katika mji mkuu wa Jordan Amman ambayo yaliwaua watu 60 mwaka 2005.
PICHA TATA YA LULU NA UJUMBE WAKE ALIOTUPIA MTANDAONI VYAWA GUMZO! 
====>>JIONEE HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA
 KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142. 
ASANTE NA KARIBU TENA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.