Harmonize amedai kuwa hakuna ushindani ndani ya lebo ya WCB wala chuki tofauti na watu wengine wanavyodhania.
Muimbaji huyo ameongeza kuwa hakuna msanii wa lebo hiyo anachukia pindi mwingine anapofanya kolabo na msanii mwingine mkubwa kwa kuwa kila mtu anakuwa na riziki yake na mafanikio ya mmoja ndio ya kwao wote.
Pia Harmonize amesema kuwa si kweli kama inavyodaiwa na baadhi ya watu kuwa wanaachia nyimbo zao kwa ajili ya kuzizima nyimbo za wasanii wengine na kudai kuwa wao wamepeana muda na kila mtu ana muda wake waliopeana kuachia nyimbo zao.
Note: Only a member of this blog may post a comment.