Ikiwa imepita miezi mitatu na siku kadhaa toka kutokea kwa tetemeko la Ardhi mkoani Kagera leo Rais wa Jamhuri wa Muungano Mh. John Pombe Magufuli anategemewa kuwasili mkoani humo kwa ziara ya siku mbili yenye lengo la kuwatembelea wananchi walioathirika na tetemeko la Ardhi lakini pia kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi kadhaa ya maendeleo ambayo yaliathiriwa kutokana na tetemeko hilo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mstapha jana alisema Rais ataingia asubuhi ya leo akitokea Geita na baadaye atahudhuria ibada ya misa na kesho yake ndiyo atawatembelea baadhi ya wananchi waliotumia nguvu zao kujenga nyumba zao na makazi baada ya kuharibiwa na tetemeko la Ardhi kisha atatembelea miradi ya ujenzi wa shule ya Sekondari ua Ihungo na kuweka jiwe la msingi na kuzungumza na wananchi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.