Monday, December 26, 2016

Unknown

Ubingwa wa VPL ni wa SIMBA SC Msimu Huu!

BAADA ya kikosi chake kufanikiwa kumaliza mwaka kikiwa kinaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara Kocha mkuu wa Simba, Joseph Omog amesema sasa ameanza kuona mwanga wa ubingwa.
Kikosi cha Simba juzi kilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu na kuzidi kujichimbia kileleni ikiwa na pointi 41 dhidi ya 37 za mabingwa watetezi Yanga walio katika nafasi ya pili.


Akizungumza na gazeti hili baada ya mchezo huo, Omog aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza kwa kujituma ingawa alikiri mchezo ulikuwa mgumu kwani wapinzani wao walionekana kuwakamia.

Simba itacheza na Ruvu Shooting Alhamisi ya wiki hii kabla ya kwenda kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Desemba 30. Yanga itacheza na Ndanda.
“Nawapongeza sana wachezaji wangu walicheza vizuri muda wote wa mchezo ingawa pia nawapongeza wapinzani wetu JKT Ruvu nao walicheza vizuri na kutupa presha muda wote wa mchezo lakini mwisho wa siku tulipata pointi tatu,”alisema Omog.


Alisema atahakikisha jitihada walizo nazo wanaziendeleza na kwenye mechi zinazofuata ili kufanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu kama walivyokusudia.

Aidha Omog, alisema kitengo cha timu yao kuanza mwaka mpya wa 2017 wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi ni dalili njema kwao ingawa ndiyo kwanza mzunguko wa pili umeanza lakini anafurahi kuona wachezaji wake wanacheza kwa kujituma na kuonesha bidii katika kila mchezo.

Kocha huyo alisema atahakikisha wanafanya kila linalowezekana ili kuendelea kupata matokeo katika mechi zao zinazofuata ili wabaki kwenye nafasi hiyo ya kwanza hadi mwishoni mwa ligi hiyo kama ambavyo wanapanga.

Alisema kitendo cha kuwaacha wapinzani wao Yanga kwa pointi nne ni moja ya ishara ambazo za timu yake kuwa mabingwa msimu huu kwani kwa kasi waliyokuwa nayo hafikirii kama wanaweza kuondoka kwenye nafasi hiyo.
“Yanga wasijidanganye kwamba wanaweza kutuondoa kwenye nafasi hii ya uongozi, kwa sababu tumekusudia kuwa mabingwa msimu huu maana tumewazidi kwa kila kitu,” alitamba Omog.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.