Monday, December 26, 2016

Unknown

Tujikumbushe Ubora wa Mbwana SAMATTA Tukiumaliza Mwaka Huu 2016

Uthubutu, kujiamini na kufanyia kazi kipaji chake, hakika ni moja ya vitu ambavyo vimemfanya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Genk ya Ubeligji Mbwana Samatta aendelee kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika tasnia ya michezo.

Mwaka 2016 hauwezi kusahaulika kwenye ramani ya soka nchini kutokana na mafanikio aliyopata Mbwana Samatta akianza na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ligi za ndani iliyotolewa Januari 7 pale Abuja Nigeria. Baada ya hapo alitua katika klabu ya KRC Genk ya Ubeligji ambapo alianza kwa mafanikio akfunga mabao katika mechi zake za awali.
Akiwa Genk Samatta amekuwa Mtanzania wa kwanza kucheza michuano ya Europa akiisaidia timu yake kusonga mbele kutoka hatua ya awali ya makundi hadi hatua ya 32 bora ikiwa kama kinara wa kundi mbele ya timu kongwe kama Athletic Bilbao.

Kila la kheri Samatta na timu yako huenda mwaka 2017 tunaweza kuketi kukutazama kwenye runinga zetu ukikipiga UEFA na sio Ueropa tena.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.