Polisi Waliomdhalilisha Mchungaji wa KKKT Kwa Kumvua Nguo, Kumpiga Picha na Kutaka Milioni 10 Wakufuzwa Kazi!
Askari polisi wanne mkoani Kilimanjaro waliotuhumiwa kutengeneza tukio la ushoga kwa mchungaji wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania(KKKT) wamefukuzwa kazi.
Polisi hao walidaiwa kumkamata mchungaji huyo na mwanaume mwingine katika nyumba ya kulala wageni wilayani Hai, kumshurutisha avue nguo, kumpiga picha na kudai awalipe shilingi milioni 10.
Hata hivyo mchungaji huyo ambaye jina lake limehifadhiwa aliwalipa shilingi 5.4 milioni polisi hao kumuachia baada ya kumshikilia kwa masaa sita.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Note: Only a member of this blog may post a comment.