Friday, December 23, 2016

Unknown

Mwanamuziki Mkongwe Celine Dion Apiga Chini Ofa ya Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump

Muimbaji mkongwe wa nyimbo za taratibu kutoka Canada, Celine Dion ameongeza idadi ya wasanii waliopiga chini ofa ya kutumbuiza kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Celine alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliotakiwa kutumbuiza kwenye sherehe hizo zitakazofanyika Januari 20 mwakani lakini uongozi wake umekataa ofa hiyo kutokana na ratiba za show kumbana msanii huyo.

Chanzo kimoja kimeuambia mtandao huo kuwa siku ya sherehe hiyo Celine atakuwa akifanya show kwenye ukumbi wa Caesars Palace mjini Las Vegas. Msanii mwingine aliyekataa kufanya show kwenye sherehe za kuapishwa kwa Trump ni Elton John.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.