KADA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Khamis Mgeja amewaomba Watanzania kumsamehe waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa kushindwa kuwashukuru baada ya uchaguzi mkuu.
Ametaka wajue kuwa kada huyo aliyehamia Chadema baada ya kukatwa jina lake kwenye orodha ya wagombea urais wa CCM, sasa yupo kwenye kifungo cha kisiasa kutokana na Serikali kuzuia mikutano ya hadhara.
Mgeja alitoa kauli hiyo jana katika Kata ya Tumbi Manispaa ya Tabora wakati alipokuwa akiongea na wanachama na viongozi mbalimbali wa Chadema, pamoja na wananchi wachache waliovamia kikao.
Mgeja alisema anasikitishwa na kitendo cha Lowassa kuzuiwa kuwashukuru wananchi waliompigia kura kupitia mikutano ya hadhara na bado anaamini kuwa hawakumtendea haki.
“Nawaombeni ndugu zangu Watanzania mliopiga kura nyingi na za kishindo kwa mzee wetu Lowassa, kura zaidi ya milioni sita, mtusamehe kwa yeye kushindwa kuwashukuru. Serikali imeminya uhuru wa demokrasia kwa kuzuia mikutano ya hadhara,” alisema.
Alisema Lowassa anapenda sana kuwafikia wananchi kupitia mikutano ya hadhara ili awashukuru kwa heshima kubwa waliyompa, lakini ameshindwa kutokana na mikutano hiyo kuzuiwa.
Hata hivyo, alibainisha kuwa Lowassa hatachoka kuwasemea wananchi hao kero zao na ana imani kero hizo Rais Magufuli na viongozi wa CCM wanazisikia na watazifanyia kazi.
Kada huyo wa Chadema na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, alisema wananchi wanapaswa kumuelewa Lowassa na Ukawa kwa jumla kuwa wanapenda kufanya mikutano ya hadhara ila wamezuiwa.
Alisema viongozi wanapenda kuwafikia wananchi ili kusikiliza changamoto zao za maisha, pia kuzungumza pamoja kuhusu mustakabali wa nchi, lakini hilo sasa ni gumu kufanyika.
“Sisi wachambuzi wa kisiasa tunaona dhahiri kabisa ishara ya kifungo cha kisiasa kwa Lowassa na viongozi wa vyama vya upinzani nchini. Haya yamefanywa makusudi na watawala ili kuminya demokrasia,” alisema.

Note: Only a member of this blog may post a comment.