Mwanamuziki wa kundi la The Amazing, Abela, amesema Marekani ni nchi yenye changamoto nyingi kuishi kwa mtu mweusi.
“Marekani si sehemu rahisi kwa kuishi,” anasema. “Sasa hivi kuna uhasama mkubwa wa rangi Marekani, hivyo kuwa mtu mwenye rangi ni ngumu kiasi.Nina furaha kuwa nyumbani kwenye sehemu ambayo kila mtu anaelewena na mwenzie na ni nchi yenye amani,” ameongeza.
Abela anasema hata hivyo haikuwa rahisi tu kuamua kuondoka Minnesota ambako wazazi wake wanaishi kuja Dar. “Haikuwa rahisi, na ni ngumu kidogo kuwashawishi watu kwamba muziki unaweza kuwa kazi,” anaeleza.
“Kwahiyo nimekuja hapa kivyangu na nilijiamini mwenyewe, ninafurahi kuwa nilichukua uamuazi huo, haikuwa rahisi lakini ninaona matokeo, bila shaka inalipa.”
Anasema familia yake inamuunga mkono kwakuwa baba yake pia ni mtengezaji wa filamu hivyo naye ni msanii. Ameongeza kuwa wameshangaa pia kuona kile anachokifanya kimeanza kuzaa matunda tayari. -via Bongo5
Note: Only a member of this blog may post a comment.