Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba amesimamisha shughuli zote za Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza zao la Korosho (CIDTF), baada ya kubaini mfuko huo kutumia vibaya fedha za umma na kusababisha hasara.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam amesema mfuko huo umekuwa ukilalamikiwa kwa muda mrefu na wakulima na kwamba mfuko huo umebainika kutumia fedha vibaya, ikiwa ni pamoja na kutofuata maagizo ya Rais John Magufuli ya kufungua akaunti Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
“Sasa hivi nina taarifa kuwa mfuko huu katika benki moja wanazo fedha karibia sh. bilioni tano ambazo pamoja na kuiva, walielekezwa wazitoe huko na kuzipeleka BoT, lakini wameendelea kugoma, najiuliza kwa nini wamegoma,” alihoji waziri huyo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.