Kocha Arsene Wenger amesema kuwa mwanzoni alipatwa na hofu kwamba alikuwa anafanya makosa kumchezesha Alexis Sanchez kwenye nafasi ya mchambuliaji wa kati awapo uwanjani.
Pamoja nahayo yote kutokea Wenger amejipatia matunda ya uamuzi wake na sasa anaamini kwamba Sanchez ndiye mrithi wa staa wa zamani wa timu hiyo, Thiery Henry.
Kwa hivi sasa Sanchez amekuwa ni mfungaji tegemeo wa klabu ya Arsenal na anafanana na Henry kwa uwezo wake wa kupachika mabao, na kutoa pasi, chenga na mbio awapo uwanjani.
Note: Only a member of this blog may post a comment.