Thursday, October 6, 2016

Unknown

Bill Nas Afunguka Kuhusu Kujiunga na Lebo ya WCB ya Diamond Platinumz

Msanii wa Hip Hop Bongo, Bill Nas amefunguka juu ya tetesi za kuhusishwa kujiunga na lebo ya WCB. Akiongea na kipindi cha Clouds E cha Clouds TV, rapper huyo amesema kuwa taarifa hizo si za kweli.

“WCB ni lebo kubwa kwasasa Afrika Mashariki nadhani hilo lipo wazi kabisa ila swala la mimi kwenda Wasafi aisee hata mwenyewe nimeshangaa, maana hata sijawahi kuongea na uongozi wa WCB wala sijawahi kwenda hata studio kwao, naona limekuwa kubwa hadi washikaji zangu wananipigia simu wakiniulizia lakini si kweli kabisa hilo swala,” alisema Bill Nas.
Kwa sasa Bill Nass anafanya vizuri na ngoma yake Chafu Pozi.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.